Mabingwa wa soka Tanzania bara Simba wamemaliza hatua ya makundi ya michuano ya kombe la Mapinduzi kwa kuichapa Mlandege Fc bao 1-0 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Amaan Jumanne usiku.
Bao pekee la Simba liliwekwa kimiani kwa mkwaju wa penati na kiungo Haruna Niyonzima
Simba imetinga hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo kwa ushindi wa asilimia 100.
Baada ya mchezo huo kikosi cha kwanza cha Simba kinarejea jijini Dar es salaam kesho kuendelea na maandalizi ya mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya JS Sauora utakaopigwa Jumamosi, Januari 12 2019.
Aidha wachezaji wa kikosi cha pili cha Simba (Simba B) wanatarajiwa kumalizia hatua iliyobaki ya michuano hiyo.
ADVERTISE HERE