Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amepania hasa kuhakikisha timu hiyo inarejesha makali yake ya kutoa vipigo kwa kila itakayekutana nae kwenye ligi.
Kocha huyo anayependelea kutumia mfumo wa kushambulia na kuzuia kwa pamoja 'Toto Football' ameanza kupata mwanga wa kikosi chake.
Aidha Zahera amesema amevutiwa na viwango vya wachezaji wapya waliosajiliwa na Yanga na pengine atakuwa na wakati mgumu kupata kikosi cha kwanza.
Kocha huyo Mcongoman aliye na uraia wa Ufaransa amesema kama wachezaji wote wapya alionao mkoani Morogoro wangekuwa wamesajiliwa kwa ajili ya michuano ya CAF, wasingepoteza michezo miwili dhidi ya Gor Mahia kirahisi.
Zahera amefichua kuvutiwa zaidi na kiungo mpya mwenye umri wa miaka 19 Feisal Salum 'Fei Toto' na kubainisha kuwa atamtumia kiungo huyo sambamba na Papi Tshishimbi.
Fei Toto tayari anaonekana kuyazoea maisha ya Jangwani na anatabiriwa atakuwa msaada mkubwa kwa Yanga msimu huu licha ya umri wake mdogo.
Deus Kaseke na Mrisho Ngassa ni wachezaji wengine ambao tayari wanaonekana kuwa ndani ya mipango ya Zahera.
Kaseke aliongezwa kwenye kikosi cha Yanga kinachoshiriki michuano ya CAF ambapo kwenye mchezo dhidi ya Gor Mahia uliopigwa Dar aliifungia Yanga bao lake la kwanza kwenye michuano hiyo.
Ngassa amekuwa kivutio mazoezini, kasi yake imempagawisha Mcongomani huyo na kufichua kuwa atamtumia na Kaseke nafasi za ushambuliaji wa kutokea pembeni.
Mohammed Issa 'Banka' ni mchezaji mwingine ambaye huenda akaingia moja kwa moja kwenye kikosi cha Zahera.
Banka kwa sasa hayuko kambini mkoani Morogoro akiwa na ruhusa baada ya kupata udhuru. usajili wake ulipendekezwa na Zahera mwenyewe.
August 12 Yanga itacheza na Mawenzi FC kwenye mchezo wa kumuaga mkongwe Nadir Haroub 'Cannavaro' aliyetundika 'daluga'.
Zahera anatarajiwa kuutumia mchezo huo kuwatambulisha wachezaji wake wote wapya kwa kuwapa nafasi na huenda akautumia mchezo huo kuwapa mashabiki 'mwanga' wa Yanga mpya.
Yanga ya Zahera inaweza kuwa hivi;

Yanga ina kikosi kipana ambacho hakuna shaka kitatoa ushindani wa kutosha kwenye ligi.
Kwani licha ya kikosi hicho hapo juu, nje bado kuna wachezaji ambao watampa wakati mgumu Zahera kuamua nani aanze.
Ibrahim Ajib, Pius Buswita, Mwinyi Haji, Raphael Daudi, Klaus Kindoki, Jaffar Mohammed, Maka Edward, Thabani Kamusoko, Yusufu Mhilu, Amissi Tambwe na Matheo Anthony wote hawa wanaweza kuingia kwenye kikosi cha kwanza.

ADVERTISE HERE