Michuano ya SportPesa Super Cup inatarajiwa kuanza Januari 22 mpaka Januari 27 2019 michezo yote ikitarajiwa kupigwa katika dimba la Taifa.
Mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba wao wataanza kampeni ya kutwaa taji la mashindano hayo kwa kuivaa AFC Leopards Januari 23 2019.

Bingwa wa michuano ya mwaka huu atajinyakulia kombe, kitita cha Dola 30,000 (zaidi ya Mil 68) na kupata tiketi ya kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Everton inayoshiriki ligi kuu ya Uingereza.
Mchezo dhidi ya Everton utapigwa jijini Dar es salaam mwezi Julai 2019 wakati wa maandalizi ya msimu mpya wa 2019/20.
ADVERTISE HERE