Nahodha msaidizi wa kikosi cha Yanga Juma Abdul amesema wana matumaini makubwa ya kufanya vizuri kwenye ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu wa 2018/19 inayotarajiwa kuanza wiki mbili zijazo.
Abdul amesema wazoezi waliyofanya mkoani Morogoro kwa karibu wiki moja sasa yamewaimarisha maradufu na wako tayari kupambana na timu yoyote.
Usajili uliofanywa na klabu ya Simba pamoja na 'mbwembwe' za viongozi na mashabiki wa timu hiyo umewafanya wengi kuamini mabingwa hao wa msimu uliopita wako kwenye nafasi nzuri zaidi ya kutetea ubingwa kwa msimu wa pili mfululizo.
Lakini Juma Abdul hafikirii kama jambo hilo litakuwa rahisi.
"Sisi tunajiandaa kikamilifu na kwa maandalizi tunayofanya, tumedhamiria kutwaa ubingwa," amesema Abdul ambaye hivi karibuni ameteuliwa kuwa nahodha msaidizi wa kikosi cha Yanga sambamba na Thabani Kamusoko wakimsaidia Kelvin Yondani aliyerithi mikoba ya Cannavaro.
"Simba kusajili vizuri haimaanishi kwamba watatwaa ubingwa. Kuna tofauti kubwa kati ya mchezaji mmoja mmoja na timu."
"Sisi tunajiandaa kama timu, na ni hivyo hivyo ndivyo tutakavyocheza ligi itakapoanza."
Yanga imesajili wachezaji saba na wote wako mkoani Morogoro wakiendelea na maandalizi ya msimu mpya.

ADVERTISE HERE