Mwekezaji wa klabu ya Simba Mohammed Dewji 'MO' amedhamiria kuipeleka Simba katika anga za Kimataifa na kuifanya kuwa moja ya timu za kuogopwa barani Afrika.
Baada ya kuwa mbioni kukamilsha ujenzi wa uwanja wa kisasa wa mazoezi, MO anatarajiwa kuwaletea basi jipya mabingwa hao wa Tanzania Bara.
MO amekuwa akimwaga mabilioni kuhakikisha anatimiza ndoto hiyo ya kuipeleka Simba kileleni mwa mafanikio barani Afrika.
Licha ya kuwepo kwa taarifa za kununuliwa kwa basi jipya, Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba Mulamu Nhambi amesema kwa sasa wanataka kumalizia kwanza ujenzi wa uwanja wa mazoezi ulioko Bunju jijini Dar es salaam.
Uwanja wa Bunju unaelezwa katika hatua za mwisho sasa ukiwa umeanza kutandazwa nyasi za bandia.
Ujenzi wa uwanja huo unatarajuwa kukamilika mwezi ujao.