Kocha wa Yanga awakubali Chama, Boko, Kagere

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
4 Jan 2019
Kocha wa Yanga awakubali Chama, Boko, Kagere

Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amekuwa maarufu sana miongoni mwa makocha wanaofundisha ligi kuu ya Tanzania Bara kutokana na tabia yake ya kuzungumza sana.

Jana wakati akihojiwa katika kipindi cha nyundo ya Baruani, mtangazaji wa kipindi hicho Baruani Muhuza alimuuliza ni wachezaji gani watano ambao anawakubali zaidi katika klabu ya Simba?

Zahera aliwataja John Bocco, Meddie Kagere na Clatous Chama 'CCC' huku akiongeza kuwa wachezaji wengi wa Simba ni wazuri lakini yeye angependelea zaidi kufanya kazi na wachezaji hao watatu.

Aidha kocha huyo ameipa Simba nafasi ya kufanya vizuri kwenye michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika akieleza kuwa kipindi hiki hakuna timu ndogo kwenye mashindano ya Afrika.

Amesema Simba ina nafasi ya kutinga robo fainali sawa na wapinzani wake Al Ahly, AS Vita na JS Saoura kinachohitajika ni kufanya maandalizi ya kutosha tu.

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
9h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
12h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’