Zahera ameshitukia upendeleo kwa Simba ratiba VPL

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
4 Aug 2018
Zahera ameshitukia upendeleo kwa Simba ratiba VPL
Kocha pekee mwenye uraia wa Ufaransa na DR Congo kwenye Ligi Kuu Bara, Mwinyi Zahera anayeinoa Yanga amesema anaona wazi kwamba Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) linataka kuibeba Simba msimu ujao wa ligi kuu kutokana na ratiba kuwa rafiki kwao.

Ratiba ya ligi kuu ambayo imepangwa kuanza kutimua vumbi Agosti 22, inaonyesha Yanga itaanzia ugenini katika michezo yake mitatu ya ugenini ambapo ni dhidi ya Mtibwa Sugar ya Morogoro itakayopigwa Agosti 23, kisha watakwenda Bukoba kuvaana na Kagera Sugar Agosti 25 halafu Septemba 2, watakwenda Shinyanga kucheza na Mwadui FC.

Lakini hata hivyo Yanga baada ya kucheza mechi na Kagera Agosti 23, watalazimika kuanza kujiandaa na safari ya kwenda Rwanda ambapo watakuwa na mechi ya hatua ya makundi ya Shirikisho Afrika dhidi ya Rayon Sports.

Simba yenyewe itacheza mechi tatu nyumbani ambazo ni dhidi ya Prisons itakayopigwa Agosti 22, kisha Agosti 25 watacheza na Mbeya City halafu Septemba Mosi watakipiga na Lipuli.

Hivi karibuni TFF ilitangaza kuwa timu mwenyeji ndiyo itakayokuwa inachukua mapato yote hali ambayo Yanga wanaona kama wanaonewa kwani hawatopata chochote kwenye mechi hizo.

Kutokana na ratiba hiyo, Zahera amesema anaona wazi kuwa TFF inataka kuibeba Simba kwani haiwezekani wao wakapangwa kucheza mechi tatu mfululizo ugenini tofauti na ilivyo kwa Simba na Azam ambao ni wapinzani wao wa karibu ambao wao watacheza mechi tatu nyumbani.

β€œNi mara ya kwanza kuona kitu hiki kinatokea dunia nzima, huwezi kuanza kucheza mechi tatu ugenini huku wenzako ambao mnapigania kuwania kombe wanaanzia nyumbani.

β€œHii inaonyesha wazi kuwa TFF inaisaidia timu ya Simba, sijui kwa nini wamefanya hivi inaumiza kwa nini Azam na Simba waanzie nyumbani mechi tatu na sisi ugenini tu, kuna sababu gani,” aliwaka Zahera.

Championi
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
3h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
8h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
12h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
13h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
13h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
17h ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’