Bao la tatu lililofungwa na Mashujaa Fc na kuiondosha Simba katika michuano ya kombe la FA ni makosa ya mlinda lango Deogratius Munishi 'Dida' kwa asilimia 100.
Mpira uliopigwa na mshambuliaji wa Mashujaa Fc Rajabu Athumani ulikuwa hauonekani kuwa na madhara lakini ulimpita Dida mikononi mwake na kuserereka wavuni.
Aidha kiwango kilichoonyeshwa na mlinda lango huyo aliyesajiliwa na Simba mwanzoni mwa msimu akitoka Afrika Kusini, hakikuwa cha kuridhisha.
Huenda benchi la ufundi la Simba likalazimika kuanza kumuamini mlinda lango namba tatu Ali Salim kuwa mbadala wa Manula kwani tangu atue, Dida ameshindwa kuonyesha makali yake.
ADVERTISE HERE