Kessy akanusha taarifa za mtandaoni

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
29 Jul 2018
Kessy akanusha taarifa za mtandaoni
Beki wa zamani wa Yanga Hassani Kessy amekanusha kutoa taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii akiutuhumu uongozi wa Yanga kuhusu usajili wake.

Kessy amesema uamuzi wa kuondoka Yanga uliafikiwa na pande zote mbili.

"Nasikitika sana kuona kuna mtu katengeneza maneno juu yangu na kuyasambaza mtandaoni. Sijaongea lolote tangu usajili umefungwa, " amesema Kessy.

"Kilichotokea kati yangu na Yanga ni maelewano tu na sina kinyongo nao kabisa.

"Mtazamo wangu mkubwa ni kucheza nje ya nchi na nashukuru mambo yanaendelea vizuri. Yanga walinipokea vizuri na mpaka mkataba unakwisha tulikuwa vizuri.

"Nawahesabu kama sehemu ya familia yangu. Hivyo naomba sana mtu asipotoshe kilichopo kati yangu na Yanga kwa masilahi yake binafsi . Sina kinyongo na timu yoyote ile , mimi ni mchezaji na maisha popote," amesema Kessy.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
2h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
8h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
18h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
23h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’