Kila la kheri Simba, kila la kheri Mabingwa wa nchi

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
23 Dec 2018
Kila la kheri Simba, kila la kheri Mabingwa wa nchi

Mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba leo Jumapili Disemba 23 2018, saa kumi jioni wanashuka kwenye uwanja wa Taifa kuikabili Nkana Fc katika mchezo wa marudiano wa ligi ya mabingwa barani Afrika, raundi ya kwanza.

Baada ya kupoteza kwa mabao 2-1 katika mchezo wa kwanza uliopigwa nchini Zambia wiki iliyopita, Simba ina nafasi ya kupindua matokeo leo na kutinga hatua ya makundi ya michuano hiyo mikubwa kabisa barani Afrika baada ya AFCON.

Ushindi wa bao 1-0 utatosha kuwavusha mabingwa hao wa nchi kwenda makundi.

Ni mchezo ambao ulikuwa ukisubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka nchini. Siku ya leo mashabiki wa Simba hawahitaji kingine zaidi ya kuiona timu yao inatinga hatua ya makundi.

Viingilo vya mchezo huo 'vilirahisishwa' ili kuwapa nafasi mashabiki wengi kujitokeza kwa wingi uwanja wa Taifa ili kuipa sapoti Simba kuhakikisha inapata matokeo ya kuweza kuivusha hatua inayofuata.

Majukwaa ya VIP viingilio ni Tsh 20,000/- Tsh kwa Tsh 10,000/- wakati upande wa mzunguuko kiingilio ni Tsh 3,000/- tu.

Mgeni rasmi katika mchezo huo atakuwa Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mh. Joseph Kakunda.

KILA LA KHERI WEKUNDU WA MSIMBAZI

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
13h ago
READ MORE β†’
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
13h ago
READ MORE β†’
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
16h ago
READ MORE β†’
Makundi CAFCL kujulikana leo
Makundi CAFCL kujulikana leo
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
21h ago
READ MORE β†’
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
1d ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
1d ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
1d ago
READ MORE β†’