Baada ya ushindi wa jana wa mabao 2-1 dhidi ya KMC, kikosi cha Simba leo kimeendelea na program ya mazoezi kujiandaa na mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Nkana FC.
Mazoezi ya mabingwa hao wa Tanzania Bara yanafanyika kwenye uwanja wa Boko Veterans yakisimamiwa na kocha Mkuu wa timu hiyo Patrick Aussems.
Simba inakiandaa kikosi chake kikamilifu kuhakikisha kinaibuka na ushindi katika mchezo huo utakaopigwa Jumapili, Disemba 23 kwenye uwanja wa Taifa
Ushindi wa bao 1-0 utatosha kuivusha Simba kwenda hatua ya makundi.
Uongozi wa Simba umeanzisha kampeni ya KUFA NA KUPONA kuwahamasisha mashabiki wajitokeze kwa wingi Jumapili ili kuujaza uwanja wa Taifa unaochukua watazamani takribani elfu 60
Katika michezo muhimu kama hii sapoti ya mashabiki ina mchango mkubwa kwa wachezaji katika kuwainua na kuwafanya waipiganie timu iweze kupata matokeo

ADVERTISE HERE