Baada ya mwafaka kufikiwa baina ya wachezaji na viongozi jana, kikosi cha Yanga huenda kikaelekea mkoani Morogoro kuweka kambi kabla ya kuivaa Gor Mahia Jumapili ijayo.
Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera ametaka wachezaji kuwekwa sehemu tulivu ili kuwarejesha mchezoni kabla ya kuivaa Gor Mahia.
Yanga imekuwa na kawaida ya kuweka kambi mkoani Morogoro. Baadhi ya viongozi wa timu hiyo wamependekeza timu iende mkoani humo.
Wachezaji wote wamekubali kurejea mazoezini baada ya uongozi wa Yanga kuwahakikishia kuwa wanashughulikia madai yao.
Tangu warejee kutoka Kenya Alhamisi iliyopita, wachezaji waligoma kufanya mazoezi.

ADVERTISE HERE