Aussems kutumia mbinu za eSwatini kuiua Nkana Fc kwao

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
10 Dec 2018
Aussems kutumia mbinu za eSwatini kuiua Nkana Fc kwao
Kikosi cha mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba kinatarajiwa kuondoka kwa awamu mbili keshokutwa Jumatano na Alhamisi alfajiri kwenda nchini Zambia kwa ajili ya mchezo wa kwanza wa ligi ya mabingwa dhidi ya Nkana Fc.

Mchezo huo wa raundi ya kwanza utapigwa Jumamosi, Disemba 15 huko Kitwe Zambia.

Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems amesema wanakwenda Zambia wakiwa na lengo la kushinda mchezo huo ili kujirahisishia kazi kwenye mchezo wa marudiano utakaopigwa uwanja wa Taifa wiki moja baadae.

Aussems ambaye anaendelea kuwaandaa vijana wake katika uwanja wa Boko Veterans, amesema watatumia mbinu walizotumia kwenye mchezo waliocheza eSwatini dhidi ya Mbabane Swallows

Katika mchezo huo ambao Simba iliibuka na ushindi wa mabao 4-0, ni mabingwa hao wa Tanzania waliotawala mchezo kwa muda mwingi na kuwafanya wenyeji wao waonekane kama wageni katika dimba lao.

Aussems ametamba kuwa yeye sio mfuasi wa soka la kujilinda kwani anaamini njia sahihi ya kujilinda ni kumiliki mpira na sio kuweka wachezaji wengi nyuma

Nae Katibu Mkuu wa Simba Dr Arnold Kashembe amesema maandalizi ya safari ya Zambia yamekamilika na wanatarajia msafara wa kwanza utaondoka keshokutwa Jumatano.

Dk Kashembe amesema tayari wametuma wawakilishi wao nchini Zambia kwa ajili ya kuweka mazingira sawa na mapokezi ya kikosi cha Simba ambacho kitafanya mazoezi nchini Zambia kwa siku mbili kabla ya mchezo
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
5h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
17h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
22h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’