Sikia tambo za kocha wa Prisons

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
•
18 Nov 2017
Sikia tambo za kocha wa Prisons
Baada ya mchezo mmoja wa ligi kuu ya Vodacom uliopigwa leo kuishuhudia Singida United ikiilaza Lipuli bao 1-0, michezo kadhaa ya ligi hiyo itapigwa kesho Jumamosi.

Mchezo unaosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka ni mchezo kati ya Prisons dhidi ya Simba.

Kuelekea mchezo huo, kocha wa Tanzania Prisons, Mohammed Abdalah amesema kwamba Simba siyo timu kubwa, bali ni timu kongwe na haiwatishi chochote.

Abdallah amesema kwamba lengo lao ni kushinda na kurudia kile walichokifanya msimu uliopita dhidi ya Wekundu hao wa Msimbazi walipowachapa 2-1 Uwanja wa Sokoine.

“Tumejipanga vya kutosha kuchukua pointi tatu katika mchezo wetu dhidi ya Simba, ningependa tuondoshe hayo mawazo eti tunacheza na timu kubwa, sisi tunajua tunacheza na timu kongwe. Simba wao watakuwa na wachezaji 11, na sisi tutakuwa na wachezaji 11. Kila mwalimu kaandaa mbinu zake, tutapambana uwanjani,”amesema.

Abdallah amesema kikosi chake kipo vizuri na hakina majeruhi hata mmoja, baada ya kambi yao ya wiki moja Kahama na Iringa, wakitokea mkoani Kagera, ambako Novemba 4 walitoa sare ya 1-1 na wenyeji, Kagera Sugar uwanja wa Kaitaba katika mchezo mwingine wa Ligi Kuu.

Amesema katika kambi yao ya siku nne Kahama walipata pia na mchezo wa kirafiki wa kujipima nguvu dhidi ya Kabela City uliomalizika kwa sare ya 1-1 Alhamisi iliyopita kabla ya kwenda Iringa, ambako wanaondokea kuingia Mbeya kwa ajili ya mchezo na Simba kesho.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
9h ago
READ MORE →
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
15h ago
READ MORE →
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
18h ago
READ MORE →
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
21h ago
READ MORE →
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
21h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
22h ago
READ MORE →
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE →
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE →
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE →
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE →