Yanga ilikamilisha zoezi la usajili mapema kabla ya jana, siku ambayo ndiyo ilikuwa tamati ya zoezi hilo.
Usajili pekee ambao ulikuwa haujafanyiwa maamuzi ilikuwa ile nafasi moja ya mchezaji wa Kimataifa pamoja na kuangalia sehemu zenye mapungufu.
Hata wakati anazungumza na waandishi wa Habari wiki iliyopita, Katibu Mkuu Charles Mkwasa alisema usajili ulikuwa umekamilika kwa asilimia 90, uongozi ulikuwa ukikamilisha mambo madogo madogo tu.
Hivyo nadhani WanaYanga tusiwe na wasiwasi na kikosi chetu. Yanga itakuwa imara sana, ni muda tu.
Tusiamini sana taarifa nyingi zinazoripotiwa kwenye mitandao ya kijami. Kuna baadhi ya wachezaji wameandikwa sana kwenye mitandao kuwa wanatua Yanga kumbe sivyo.
Mwaka huu Yanga imekuja na utaratibu mzuri kuwa taarifa sahihi kuhusu usajili zinatolewa na kitengo cha Habari na Mawasiliano pekee.
Uongozi umesema Yanga imesajili wachezaji wake wote iliyowahitaji, pia kuna wachezaji kadhaa wamepandishwa kutoka kikosi cha pili.
Naamini usajili uliofanywa na Yanga ni makini, mwaka huu Yanga imesajili wachezaji na sio majina ya wachezaji.
Kikosi cha Yanga cha msimu huu tutakishusha hapa hapa, kila mtu atakiona lakini wachezaji karibu wote tayari tumeshawafahamu.

ADVERTISE HERE