Jana baada ya mchezo wa ligi ya Mabingwa, Balozi wa heshima wa Tanzania nchini Eswatini Joseph Ndawala aliwaalika viongozi na wachezaji wa klabu ya Simba waliokuwa katika msafara wa timu hiyo kwenye hafla maalumu ya kuwapongeza nyumbani kwake.
Katika hafla hiyo Balozi Ndawala aliwapongeza wachezaji kwa ushindi mkubwa waliopata dhidi ya Mbabane Swallows.
Ndawala amewataka wachezaji waongeze juhudi ili waweze kufanya vizuri katika michezo inayofuata kwenye michuano hiyo.

Naye nahodha wa kikosi cha Simba John Bocco amewashukuru mashabiki waishio nchini humo na maeneo ya jirani waliojitokeza kwa wingi kuiunga mkono Simba
Bocco amesema sapoti yao iliwaongezea nguvu na kujihisi kama hawapo ugenini. Amesema tukio hilo limedhihirisha jinsi Watanzania tulivyo wamoja

ADVERTISE HERE