MO akoleza moto ubingwa wa Afrika

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
5 Dec 2018
MO akoleza moto ubingwa wa Afrika
Mwekezaji wa klabu ya Simba Mohammed Dewji 'MO' amewapongeza wachezaji wa timu hiyo baada ya kufanikiwa kutinga raundi ya kwanza ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika.

Simba imeiondosha Mbabane Swallows katika hatua ya awali ya michuano hiyo kwa ushindi wa jumla wa mabao 8-1

MO amesema ushindi wa jana ni ishara kwamba mabingwa hao wa Tanzania Bara wako tayari kupambana na vigogo wengine wa Afrika kuwania ubingwa wa bara hili

"Hongera Simba ya Africa. Sasa tuendelee na maandalizi ya mchezo unaofuatia, Mungu atutangulie. Narudia tena, lengo letu ni kuwa mabingwa wa Africa," ameandika MO kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Instagram

Mwanzoni mwa msimu uliopita wakati wa tamasha la SIMBA DAY, MO alitoa ahadi ya kuijenga Simba imara itakayokuwa na uwezo wa kushindana sio Tanzania pekee bali Africa nzima

Ahadi hiyo ameikamilisha kwa kiasi kikubwa kwani licha ya usajili wa wachezaji mahiri, Simba imemleta kocha Patrick Aussems ambaye ametengeneza timu imara ambayo imeonyesha kuwa tayari kuchuana na timu yoyote barani Afrika.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
9h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
13h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’