Kwa yanayoendelea ndani ya uongozi wa Yanga sasa ni dhahiri kuwa mambo hayako sawa na uongozi wa klabu hiyo unapaswa kuwaambia ukweli wapenzi na wanachama wake kabla mambo hayaja haribika zaidi.
Tangu kuondoka kwa Manji, uongozi wa Yanga chini ya Kaimu Mwenyekiti wake Clement Sanga umekuwa hauweki wazi masuala mengi yanayoikabili klabu hiyo.
Msimu uliomalizika wachezaji wa Yanga walipita katika mazingira magumu ikielezwa kuna kipindi walikosa mishahara mpaka miezi mitatu hali iliyopelekea baadhi wakaendesha migomo.
Uongozi wa Yanga uliishia kukanusha uwepo wa changamoto hiyo ambayo imechangia kwa kiasi kikubwa Yanga kumaliza nafasi ya tatu msimu uliomalizika wa ligi kuu ya Vodacom.
Baada msimu kumalizika ikaelezwa kuna wachezaji saba tu waliokuwa na mikataba Yanga lakini taarifa iliyokuwa imetolewa awali ilisema ni wachezaji 10 tu ambao mikataba yao ilikuwa imemalizika.
Mchakato wa usajili wa klabu ya Yanga nao umekuwa wa kusuasua viongozi wakidai hawaweki wazi wachezaji wanaowasajili kwa kuwa baadhi ya timu hasa Simba zimekuwa zikiwawahi wachezaji wao.
Lakini ukweli umekuja kubainika kuwa tatizo kubwa ni ukosefu wa fedha za kuendesha zoezi la usajili licha ya kuwa uongozi umekuwa ukitoa taarifa kuwa zoezi hilo linaendelea vizuri.
Baada ya Mkutano Mkuu wa Wanachama uliofanyika Juni 10 jijini Dar es salaam, Bodi ya Wadhamini ya Yanga iliunda Kamati ya Mpito iliyopewa jukumu la kuivusha Yanga katika kipindi hiki cha mpito.
Hata hivyo ni jana tu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Abbas Tarimba amejiuzulu wadhifa wake akiwatuhumu viongozi wa Yanga kutoipa ushirikiano Kamati yake.
Tarimba amekwenda mbali kwa kumlaumu Makamu Mwenyekiti wa Yanga Clement Sanga ambaye anadaiwa kuivunja Kamati hiyo kimyakimya bila kuwapa taarifa.
Tarimba amebainisha kuwa Sanga na viongozi wenzake wanaoiongoza Yanga sasa ni 'wasanii' kwani wamekuwa wakimfuata ofisini kwake wakitaka utatuzi wa masuala mbalimbali yanayohusu fedha lakini wakitoka wanaibeza Kamati yake kwa kusema haina msaada wowote kwa Yanga.
Tarimba ameamua kutojihusisha na Yanga wakati huu wa uongozi wa akina Sanga mpaka pale Mkutano Mkuu wa Wanachama utakapoitishwa tena.
Pia swala jingine lenye ukakasi ni kurejea kwa Mwenyekiti Yusufu Manji.
Makamu Mwenyekiti Sanga amesema Manji amekubali kurejea Yanga lakini amehitaji apewe angalau miezi mitatu ili aweze kuweka baadhi ya mambo yake sawa.
Lakini kauli hiyo ilipaswa kutolewa na Manji mwenyewe kwani hakuna mwenye uhakika kama ni kweli Manji ametoa ahadi hiyo.
Wapo wanaoingia wasiwasi kuwa isije ikawa janja ya viongozi kwani ni kawaida yao kumtumia Manji kama kichaka cha kujificha kila wanapoona mambo yanakwenda kombo.
Hii haitakuwa mara ya kwanza kwa WanaYanga kuaminishwa kuwa Manji yuko mbioni kurejea lakini ikawa tofauti.
Kwa hali ilivyo Wanachama wengi wa Yanga wamepoteza imani kwa uongozi wa sasa wa timu hiyo. Ni vyema viongozi wakajiuzulu kwa maslahi mapana ya Yanga kisha ukaitishwa Mkutano Mkuu kuchagua viongozi wapya.
Kazi ya kwanza ya huo uongozi mpya iwe kufanikisha swala la mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji wa Yanga kwani licha ya Wanachama kuridhia mabadiliko, mchakato huo umekuwa ukisuasua.
Kama Wanachama wa Yanga hawatachukua hatua mapema kuna kila dalili msimu ujao utakuwa na maumivu zaidi kuliko msimu uliopita.

ADVERTISE HERE