Kiwango kinachoonyeshwa na mshambuliaji wa Simba Meddie Kagere kimezivutia timu vigogo barani Afrika ambapo Meneja wa mchezaji huyo Patrick Gakumba amesema tayari kuna timu zimeweka ofa mezani.
Gakumba amesema AS Vita kutoka DR Congo na Zamalek, mabingwa wa Misri, zimejitosa kumuwania mshambuliaji huyo ambaye hata hivyo bado ana mkataba wa miaka miwili na klabu ya Simba.
Gakumba amesema Zamaleki imeweka mezani ofa ya dola 200,000 (zaidi ya Mil 460) na iko tayari kuvunja mkataba wa mshambuliaji huyo ambaye msimu huu ameifungia Simba mabao saba kwenye ligi
Hata hivyo Simba haifikirii kumuuza mshambuliaji huyo tegemeo hasa ikizingatiwa moja ya malengo ya mabingwa hao wa Tanzania Bara msimu huu ni kufanya vizuri kwenye michuano ya ligi ya mabingwa.

ADVERTISE HERE