Viingilio mchezo dhidi ya Mbabane Swallows hadharani

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
26 Nov 2018
Viingilio mchezo dhidi ya Mbabane Swallows hadharani
Afisa Habari wa klabu ya Simba Haji Manara ametangaza viingilio vya mchezo wa ligi ya mabingwa hatua ya awali kati ya Simba dhidi ya Mbabane Swallows utakaopigwa keshokutwa Jumatano, Novemba 28 saa kumi jioni kwenye uwanja wa Taifa.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Manara amewataka mashabiki wa Simba na wadau wote wa soka nchini kujitokeza kwa wingi dimba la Taifa keshokutwa ili kuwapa sapoti wawakilishi hao wa nchi.

"Tunakwenda kuwakabili Mbambane keshokutwa Jumatano tukijua ni timu nzuri na mabingwa wenzetu. Lakini tunajua matarajio ya Watanzania na Wanasimba kwetu. Kiukweli hatutawaangusha na tunaahidi furaha kwenu," asema Manara

Manara ametaja viingilio vya mchezo huo kuwa ni;

VIP A - 20,000/-
VIP B na C - 10,000/-
Orange - 7,000/-
Mzunguuko - 5,000/-

Wakati huo huo Manara amesema klabu ya Mbabane Swallows inatarajiwa kuwasili nchini usiku wa kuakia kesho, saa saba usiku.

Mbabane ambayo haikuwa imetoa taarifa kwa Simba juu ya ujio wao, imewasiliana na TFF kuthibitisha kuwa watawasili leo usiku.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
10h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
13h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
20h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’