Salamba aahidi kuendeleza 'moto' wa mabao Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
31 Oct 2018
Salamba aahidi kuendeleza 'moto' wa mabao Simba
Mshambuliaji Adam Salamba, amesema kitendo cha kufunga kwenye michezo miwili iliyopita kimemuongezea hamu ya kuendelea kufanya vizuri zaidi msimu huu.

Salamba amesema ameongeza kujiamini na sasa anataka kutumia vema kila nafasi atakayopewa na kocha wake kuitumikia timu hiyo.

β€œNafurahi kwa sababu napata nafasi ya kucheza na nimeanza kuonyesha kile ambacho Wanasimba wanakitaka kutoka kwangu..., ingawa muhimu ni ushindi kwa timu lakini pia ninapopata nafasi ya kufunga kwangu ni furaha zaidi,” alisema Salamba.

Salamba ambaye alijiunga na Simba msimu huu akitokea Lipuli ya Iringa, amefunga mara mbili mfululizo kwenye michezo iliyopita dhidi ya Alliance ya Mwanza na Ruvu Shooting.

Katika michezo hiyo, Simba ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 5-1 (dhidi ya Alliance) na baadaye 5-0 (dhidi ya Ruvu Shooting).

Kikosi hicho cha kocha Patrick Aussems, kitashuka tena dimbani wiki hii kuumana na JKT Tanzania ambao wameamishia mechi hiyo kwenye Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga.

Simba imefikisha pointi 23 baada ya kucheza michezo 10 ikiwa nafasi ya tatu nyuma ya Yanga na Azam fc
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
2h ago
READ MORE β†’
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
17h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
19h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
20h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
22h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
2d ago
READ MORE β†’