Zahera abariki Yanga kujitoa michuano ya Kagame

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
9 Jun 2018
Zahera abariki Yanga kujitoa michuano ya Kagame
Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera ameunga mkono uamuzi wa timu hiyo kujiondoa kwenye mashindano ya CECAFA Kagame Cup yanatotarajiwa kuanza Juni 28, jijini Dar es salaam.

Mcongomani huyo mwenye uraia wa Ufaransa amesema moja ya sababu iliyopelekea Yanga kuwa na majeruhi wengi msimu uliomalizika ni baadhi ya wachezaji wake kucheza mfululizo na kukosa muda wa kutosha wa kupumzika.

Zahera amesema majeruhi hayo yaliathiri uimara wa kikosi chake na hata kama wangeshiriki michuano ya Kagame basi wangelazimika kuongeza wachezaji kutoka kikosi cha pili.

Zahera tayari ametoa likizo kwa wachezaji wote na wanatarajiwa kurejea kambini baada ya wiki tatu kuanza maandalizi ya mchezo wa kombe la Shirikisho dhidi ya Gor Mahia utakaopigwa nchini Kenya Julai 18, 2018.

Kusajili wanne wa Kimataifa

Wakati huo huo Zahera amesema kuwa anayo majina ya wachezaji wanne wa Kimataifa ambao wanaweza kusajiliwa na Yanga kama makubaliano yatafikiwa.

Kati yao, wawili ni washambuliaji, mmoja ni kiungo na mwingine ni winga.

Baada ya kuvunja mikataba ya Fiston Kayembe na Donald Ngoma, Yanga imesalia na wachezaji watano wa Kimataifa ambao ni Youthe Rostand, Papi Tshishimbi, Thabani Kamusoko, Amissi Tambwe na Obrey Chirwa.

Wachezaji ambao bado wana mikataba ya zaidi ya mwaka mmoja ni Rostand, Kamusoko, Tshishimbi na Tambwe wakati mkataba wa Chirwa unaelekea ukingoni.

Zahera amesema huenda wakalazimika kuachana na baadhi ya wachezaji waliopo ili nafasi zao zijazwe na wachezaji wapya watakaokuwa na msaada zaidi.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
7h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
11h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
16h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
16h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
20h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’