Mashabiki wa Simba wanatembea kifua mbele baada ya timu yao kushinda kwa mabao 10 katika mechi mbili dhidi ya Alliance na Ruvu Shooting.
Simba ilianza kucheza na Alliance na kushinda mabao 5-1, kabla ya kuichakaza Ruvu Shootinga mabao 5-0, mechi zote zilichezwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Simba inaonekana kukamilika kila idara kwa sasa, lakini kocha wao Mbelgiji Patrick Aussems amesisitiza bado hajaona kile kiwango anachohitaji timu yake icheze.
Homa ya usajili wa dirisha dogo limezidi kupanda kwani zimebaki wiki mbili tu kabla ya kufunguliwa kwa dirisha hilo Novemba 15 na kila timu kupata nafasi kuongeza wachezaji na kuachana na baadhi ya wachezaji ambao hadi sasa hawajazisaidia timu zao.
Aussems katika kuhakikisha Simba inakuwa hatari zaidi ameandaa orodha ya majina ya wachezaji watano hadi sita kutoka nchi mbalimbali atakayowasilisha kwa viongozi wa Kamati ya Usajili ili kuyafanyia kazi.
Anasema katika orodha hiyo ameanza kutazama baadhi ya wachezaji wanaotoka nje ya nchi kisha atawapa nafasi wazawa ambao ataona anastahili kuichezea Simba.
"Mipango yangu katika dirisha dogo ni kuwapati kusajili kati ya wachezaji watano hadi sita, orodha ya wachezaji hao nitawapa viongozi, kati ya hao kwangu ningependa asajiliwe mmoja tu dirisha dogo kutokana na mahitaji niliyonayo.
"Nataka asajiliwe mchezaji mmoja ambaye anacheza nafasi ya straika ila awe na uwezo wa kucheza namba zote za mbele, awe na uwezo wa kufunga zaidi ya nilionao sasa yaani kama mtambo wa mabao, awe na uwezo wa kutengeneza nafasi za wengine kufunga.
"Mchezaji huyo mmoja namtaka dirisha dogo na hizi nilizozitaja ndio sifa zake, hiyo orodha ambayo naiandaa wote wapo wenye sifa hizo.
"Kama kamati ya usajili itakuwa na mipango ya kuongeza mchezaji mwingine mwenye uwezo nipo tayari, lakini kabla ya kumleta hapa nataka nimfuatilie nione kama atakuwa na faida kwenye timu," alisema Aussems.
Mwanaspoti

ADVERTISE HERE