Beki mkongwe aliyeitumikia Kagera Sugar msimu uliomalizika Juma Nyosso amepigiwa 'chapuo' na Kelvin Yondani 'Vidic' ili aweze kusajiliwa Yanga.
Yondani na Nyosso waliwahi kucheza pamoja katika klabu ya Simba.
Nyosso ni mmoja wa walinzi wa kati wasiokuwa na masihara wawapo dimbani. Jambo pekee ambalo limekuwa likimrudisha nyuma mara kwa mara ni matukio ya utovu wa nidhamu.
Hata hivyo nidhamu yake imekuwa ikiimarika tangu alipofungiwa kucheza soka kwa miaka miwili mwaka 2015 kwa tukio alilomfanyia John Bocco.
Msimu uliomalizika Yanga iliyumba sana ilipowakosa Yondani na Chikupe kutokana na ukweli kwamba beki Abdallah Shaibu 'Ninja' bado hajawa mzoefu wakati Pato na Makapu walikuwa wakitumika kwa dharura tu.
Nahodha Nadir Haroub umri umemtupa mkono, hana tena makali yakuweza kushindana na washambuliaji vijana.
Yanga inahitaji beki mwingine wa kati mwenye uzoefu.
Juma Nyosso na Serge Wawa, beki wa zamani wa Azam FC wamekuwa wakihusishwa na Yanga.
Bila shaka mmoja kati ya mabeki hao anaweza kutua Jangwani.

ADVERTISE HERE