Chama ni wa Kimataifa - Aussems

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
27 Oct 2018
Chama ni wa Kimataifa - Aussems
Kiwango kinachoonyeshwa na kiungo wa Kimataifa wa Zambia Clatous Chama katika kikosi cha Simba kimewavutia watu wengi akiwemo kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems.

Akimueleza Chama, Aussems amesema kiungo huyo ana kipaji cha hali ya juu na anaamini kama hatapunguza kasi yake aliyonayo sasa basi siku si nyingi ataondoka barani Afrika kwenda kusakata kabumbu Ulaya.

Amesema uwezo unaoonyeshwa na kiungo huyo ni mkubwa na anaamini ataisaidia Simba kufanya vizuri kwenye ligi pamoja na michuano ya ligi ya mabingwa inayotarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi ujao

"Huyu kijana ana kipaji cha hali ya juu ni hazina kwa taifa lake ninamshauri asibweteke azidi kujituma ni suala la muda tu kwake aweze kucheza kimataifa na kudumisha nidhamu kwani hicho ndicho huwashinda wachezaji wengi," alisema.

Chama tayari ameifungia Simba mabao mawili kwenye ligi na amekuwa 'injini' ya kuendesha mashambulizi ya Simba.

Kiungo huyo pia ni mchezaji wa kutegemewa wa kikosi cha timu ya Taifa ya Zambia 'Chipolopolo'
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
10h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
13h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
20h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’