Mwenyekiti wa zamani wa klabu ya Yanga Yusuph Manji ameridhia maombi ya kurejea katika klabu hiyo lakini amesisitiza ni lazima ijisafishe kwanza.
Jana Manji alikutana na Baraza la Wadhamini la klabu ya Yanga kuitikia mwaliko aliopewa ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kuelekea Mkutano Mkuu utakaofanyika keshokutwa Jumapili.
Manji amesema hafurahii kuiona Yanga ikiwa katika hali iliyopo sasa lakini akasisitiza ili kufanya mabadiliko ya kweli ni lazima wale walioifikisha klabu hiyo hapo wawajibishwe.
Aidha Manji amesema pia ni lazima Wanachama waridhie mabadiliko yatayoweza kuijenga Yanga mpya.
"Yanga ni klabu yetu sote na binafsi hii ni kama sehemu ya familia yangu. Kuiona klabu inasuasua kiasi hiki sifurahi."
"wapo waliotufikisha hapa lazima wawajibike kwa mizani ya uongozi bora ili sote tuungane kuijenga upya klabu katika misingi bora na endelevu.
"Misingi Endelevu ili yoyote yule mwenye mapenzi mema na klabu, weledi katika uongozi aweze kuiongoza," amesema Manji.
"Binafsi sina pingamizi kurejea endapo watawajibika waliotuvuruga , wanachama kuridhia kuijenga Yanga mpya yenye mtazamo chanya kimaendeleo uwanjani na miundo mbinu bora katika dhana nzima ya nguvu za kiuchumi"
Sasa kazi imebaki kwa Wanachama wa klabu ya Yanga keshokutwa kuwaondoa 'wasaliti' wote pia wale wapinga mabadiliko kwani watu hao ndio adui namba moja wa Yanga.

ADVERTISE HERE