Mlinzi wa pembeni wa Simba Shomari Kapombe ameeleza kusikitishwa na tuhuma zilizotolewa dhidi yake na Mwenyekiti wa Kamti ya usajili Zacharia Hans Poppe kuwa amekuwa akiogopa kurejea dimbani licha ya kupona majeraha yake.
Akizungumza na eFM Kapombe amesema sio kweli kwamba anaogopa mechi bali bado hajapona sawasawa.
"Mimi siwezi kucheza nikiwa majeruhi, niliwahi kucheza AzamFC nikiwa katika wakati mgumu," amesema Kapombe.
"Suala la mimi kuogopa mechi si la kweli, Hanspope asingeenda kusema kwenye vyombo vya habari bali angenifuata mimi."
"Kama wanataka kuvunja mkataba na mimi, sawa, sina shida"
Tangu ajiunge na Simba Kapombe hajawahi kucheza mchezo wowote.

ADVERTISE HERE