Kikosi cha Yanga leo kimeendelea na mazoezi yake ya maandalizi ya msimu mpya kwenye viwanja vya Highlands Park mkoani Morogoro.
Yanga iko kamili ikifanya mazoezi ya 'kufa mtu' ikiwa na wachezaji wake wote wa zamani na wapya ambao wameshakamilisha taratibu zote za usajili.

Pia Mcameroon Fernando Bongyang na Mnigeria Henry Tony Okoh bado wako kikosini na huenda hatma yao ikajulikana ndani ya masaa 72.
Maamuzi juu ya wachezaji hawa yatategemea makubaliano kati ya Yanga na Mbabane Swallows juu ya mchezaji Papi Kabamba Tshishimbi ambaye angali na mkataba wa miezi minne na Mbabane.
Kama Yanga italazimika kumsubiri Tshishimbi hadi mwezi Disemba ambapo mkataba wake ndiyo unamalizika, basi kutakuwa na ulazima wa kuwasajili wote wawili na mmoja akapewa mkataba wa muda mfupi.

ADVERTISE HERE