Kocha mkuu wa Simba, Mbelgiji Patrick Aussems ameweka bayana kwamba kwa sasa ameandaa mipango thabiti ya kuhakikisha kwamba kikosi chake kinapata matokeo kwenye michezo yao ya ligi kuu iliyobaki.
Mbelgiji huyo wikiendi hii atakuwa na kibarua cha kuiongoza Simba kupambana na Stand United kwenye muendelezo wa ligi ambao utapigwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam siku ya Jumapil.
Aussems amesema kwa sasa wana uhakika mkubwa wa kupata pointi tatu kwenye michezo yao.
“Tulikuwa tunapata ushindi lakini mara zote siyo ule mkubwa ambao watu wanautaka kwa kiwango kikubwa, kwa sasa tuna kitu ambacho tumeandaa ili tuweze kufanya vizuri.
“Tunataka kushinda na hilo ndiyo jambo kubwa hapa kila mmoja analitaka, hivi karibuni nilikuwa nawaelekeza wachezaji ni nini cha kufanya kwenye michezo yetu ijayo na naamini kwamba watakifanya kazi kuanzia sasa,” Aussems amenukuliwa na gazeti la Championi

ADVERTISE HERE