Kwa wale wanaomponda Ngassa atawajibu uwanjani

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
31 May 2018
Kwa wale wanaomponda Ngassa atawajibu uwanjani
Sio siri tena kiungo mshambuliaji Mrisho Ngassa aliyeitumikia Ndanda FC msimu uliomalizika amerejea katika klabu ya maisha yake, Yanga.

Imeelezwa kuwa Ngassa amesaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia Yanga.

Kumekuwa na mjadala mkali kwenye mitandao ya kijamii hasa baada ya Yanga kuthibitisha 'kumrejesha' Ngassa nyumbani.

Wapo wakosoaji wanaosema kwamba Yanga imekosea kumsajili kiungo huyo mshambuliaji aliyezichezea Mbeya City na Ndanda FC msimu uliomalizika.

Wengi ambao wanakosoa usajili huo nadhani hawajafuatilia maendeleo ya Ngassa tangu alipotoka Mbeya City na kujiunga Ndanda FC.

Ngassa ametoa mchango mkubwa kwa klabu ya Ndanda FC kuweza kubaki ligi kuu msimu ujao.

Akiwa na umri wa miaka 29 sasa, Ngassa bado anaonekana kuwa na uwezo mkubwa na hakuna shaka atawajibu wakosoaji wake uwanjani.

Mbali na Yanga, hapa nchini Ngassa amewahi kuzitumikia Simba na Azam FC kabla hajatimkia Afrika Kusini.

Lakini ukweli ni kwamba Ngassa alin'gara zaidi wakati akicheza Yanga pengine kuliko timu nyingine yoyote.

Sababu kuu ni moja, Ngassa ana mapenzi ya dhati na klabu ya Yanga. Wakati wote aliokuwa akicheza Yanga alitumia uwezo wake wote.

Mashabiki walimpenda na haikushangaza wengi kushinikiza winga huyo arejeshwe msimu huu.

Msimu uliopita Simba ilipomsajili Emanuel Okwi, wengi waliponda usajili wake lakini mwisho wa siku ameibuka kuwa mfungaji bora msimu huu.

Ni vyema kuweka akiba ya maneno.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
2h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
6h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
9h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
10h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
13h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
22h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’