Aussems apania kuongeza mabao Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
13 Oct 2018
Aussems apania kuongeza mabao Simba
Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems amesema amekuwa akifanyia kazi mapungufu ya timu yake hasa katika safu ya ushambuliaji kuhakikisha timu hiyo inafunga mabao mengi.

Hata hivyo Aussems amesema kwa sasa wanachohitaji zaidi ni ushindi kwenye michezo yao bila ya kujali idadi ya mabao wanayofunga.

Amekiri ni kweli Simba imekuwa ikitengeneza nafasi nyingi sana kwenye michezo yake lakini imekuwa haizitumii ipasavyo changamoto ambayo anaifanyia kazi.

"Kwa sasa tunataka timu yetu ishinde hatujali ni kwa mabao mangapi. Wale wanaotukosoa kwamba timu yetu haifungi mabao mengi nawakumbusha kuwa kinachohitajika zaidi ni ushindi," amesema Aussems.

"Hata hivyo ni kweli tumekuwa na ufanisi mdogo langoni ukilinganisha na idadi ya nafasi tunazozitengeneza kwenye kila mchezo."

"Hilo tunalifanyia kazi," amesema.

Aidha, baada ya kuondolewa kwa kocha Msaidizi Masudi Djuma, Aussems amesema anataka mbadala wa Djuma awe na uzoefu wa soka la Tanzania lakini pia awe kiunganishi kizuri kati ya wachezaji na benchi la Ufundi.

Simba imeendelea kujifua kwenye uwanja wa boko Veterans kujiandaa na michezo ijayo ya ligi kuu ya Tanzania Bara licha ya kuwa ligi imesimama kupisha michezo ya timu za taifa.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
5h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
17h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
23h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’