Jana jioni timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' ilifanya mazoezi ya mwisho kwenye Uwanja wa Taifa wa Cape Verde kujiandaa na mchezo wa kutafuta tiketi ya kucheza Fainali za Africa mwakani dhidi ya wenyeji wao, Cape Verde.
Mchezo huo utapigwa leo Ijumaa, Oktoba 12, 2018 saa mbili usiku kwa saa za Tanzania
Timu hizo zitarudiana Oktoba 16,2018 Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
"Wachezaji wako tayari, na hata sisi benchi la ufundi tuko tayari. Wachezaji wameahidi kufanya kitu kizuri kwa ajili ya nchi yao," amesema Kocha Mkuu wa timu hiyo Emmanuel Amunike.
"Nimeridhishwa na utayari wa wachezaji wangu kwa ajili ya mchezo wa leo. Wana morali na nidhamu ya hali ya juu na wameonyesha kuwa na kiu ya kuipa mafanikio timu yao"
"Tunafahamu tuko ugenini, mashabiki wetu hawatakuwa wengi uwanjani lakini tuna uhakika watakuwa kwenye televisheni zao wakitutizama"
"Tunaahidi hatutawaangusha," amesema Amunike.

ADVERTISE HERE