Matokeo ya sare ya mabao 2-2 iliyopata Yanga dhidi ya Ruvu Shooting jana yanaufanya mchezo wa mwisho wa mabingwa hao wa zamani dhidi ya Azam FC kuwa na umuhimu wa kipekee.
Afisa Habari wa Yanga Dismas Ten amesema timu hiyo imejipanga kumaliza msimu kwa kishindo. Ushindi katika mchezo huo utatosha kuwafanya wamalize nafasi ya pili.
Yanga imefikisha alama 52 wakati Azam Fc ina alama 55 lakini ushindi utaifanya Yanga iipiku Azam kutokana na kuwa na uwiano mzuri wa mabao.
Ten amesema Yanga itaivaa Azam FC keshokutwa May 28 saa mbili usiku ikiwa na kikosi chake kamili baada ya wachezaji wake wote waliokosekana michezo iliyopita kutokana na sababu mbalimbali kurejea kikosini.
Katika mchezo kwanza timu hizo zilipokutana kwenye dimba la Azam Conmplex, Chamazi Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 2-1.

ADVERTISE HERE