Uongozi wa klabu ya Simba leo uliahirisha mazoezi ya timu ili kutoa fursa kwa wachezaji na benchi la ufundi kushiriki katika dua na sala maalum ya kumuombea Mwekezaji wa klabu hiyo Mohammed Dewji ambaye alitekwa mapema leo na watu wasiojulikana.
Msemaji wa klabu ya Simba Haji Manara amewataka Watanzania wote wanaoitakia mema nchi yetu wamuombee Mo ameweze kupatikana akiwa salama.
"Uongozi wa klabu ya Simba kwa mashauriano na Benchi la Ufundi la klabu yetu,chini ya Kocha Mkuu Patrick Aussems limeamua kuhairisha mazoezi ya Timu leo,ili kutoa fursa kwa Wachezaji na Benchi la Ufundi kushiriki ipasavyo kwenye Dua na Sala kwa ajili ya kiongozi wetu MO.
"Tunawaomba tena na tena watanzania na wanoitakia mema nchi yetu wasiache kumuombea uhai na uzima Bwana Mohammed Dewji"

ADVERTISE HERE