Aussems kupangua kikosi Simba mchezo dhidi ya African Lyon

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
5 Oct 2018
Aussems kupangua kikosi Simba mchezo dhidi ya African Lyon
Kikosi cha Simba, kesho Jumamosi kitavaana na African Lyon katika mfululizo wa mechi za Ligi Kuu Bara, huku Kocha Mkuu wa timu hiyo akipewa mchongo wa kubadilisha mfumo wake, huku ikielezwa kuna uamuzi mgumu anatarajia kuufanya.

Uamuzi huo, Patrick Aussems una lengo la kutaka kuiona Simba ikifika wanakotaka hasa kutetea taji lao la Ligi Kuu na kufika mbali katika mechi za kimataifa, kama moja ya masharti aliyopewa wakati akisaini mkataba Msimbazi Julai mwaka huu.

Hatua ya kocha huyo kutaka kufanya uamuzi hayo magumu yanaweza kuwapa wakati mgumu baadhi ya nyota wa klabu hiyo na ishu imekuja huku aliyekuwa mmoja wa wasaili wa kocha huyo, Dk Mshindo Msolla kumshauri abadilishe mfumo ili anyookewe Simba.

Msola alisema Simba imevuna alama tano katika mechi nne zilizopita kwa sababu ya kutokuwa na mbinu mbadala timu yake inapolemewa, hasa kuamua kumuacha Msaidizi wake, Masoud Djuma katika mechi tatu zilizopita za ugenini na kuvuna alama nne tu.

Mechi ya mwisho ya ligi Aussems kuwa na msaidizi wake ni ya Yanga iliyoisha kwa suluhu na Kocha Msolla amesema Aussems anapozidiwa hukosa njia mbadala ya kupata ushindi kutokana na mfumo wake anaoutumia wa 4-4-2.

Msolla alisema ili Simba watetee ubingwa ni lazima benchi la ufundi liwe na umoja na ushirikiano katika kushauriana mambo mbalimbali ya kiufundi ndipo watafikia malengo.

β€œBahati nzuri nimeangalia mechi zote za Simba hata wakipata ushindi lakini wanapata ushindi wa mabao machache, Aussems ni kocha mzuri ila ana tatizo moja la kushindwa kuwa na mpango wa pili pale anapoona upatikanaji na mabao ni mdogo.

β€œHata mechi ya Yanga walicheza mpira mzuri lakini hakuweza kupata ushindi na ni tatizo ndani ya Simba ambapo kocha mwingine anasoma mchezo na kubadilisha mfumo ila kwa Aussems hayupo hivyo hana mbinu mbadala, hilo litamsumbua sana anapaswa kubadilika, Simba wanahitaji matokeo mazuri kulingana na malengo yao,” alisema Dk Msolla.

Licha ya Kocha Aussems kusisitiza kuwa, atakomaa na mfumo aliotumia dhidi ya Yanga, lakini inaelezwa katika mechi ya kesho atafanya uamuzi mgumu katika kupangua kikosi chake ili kutengeneza njia ya kutetea taji lao msimu huu.

Habari za ndani zinasema kuwa, nyota waliokuwa hawaanzi kikosi wakiwamo Haruna Niyonzima na Juuko Murshid ameanza kuwapigia hesabu ya kuwatumia, hatua inayofanya baadhi ya nyota wa kikosi cha kwanza kupanguka.

β€œKocha ameanza kuona ugumu wa Ligi na sasa anataka kufanya uamuzi mgumu ndani ya kikosi chake ili kuhakikisha malengo ya kutetea ubingwa na kufanya vyema katika mechi za kimataifa zinafanikiwa,” alisema mmoja wa viongozi wa Simba aliyeomba kuhifadhiwa jina.

Mbelgiji huyo tangu atue Simba amekuwa akitumia wachezaji karibu wale wale wa kikosi cha kwanza ukiondoa Emmanuel Okwi, John Bocco na Meddie Kagere wanaobadilishana, lakini kwa kilichoelezwa mipango yake sasa ni kuona wengine wanapata nafasi zaidi.

Mwanaspoti
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
7h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
10h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
17h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’