Kagere, Okwi, Kichuya kuibeba Simba leo

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
30 Sep 2018
Kagere, Okwi, Kichuya kuibeba Simba leo
Nahodha John Bocco atakosekana kwenye mchezo wa leo dhidi ya Yanga akitumikia adhabu ya kadi nyekundu aliyopewa kwenye mchezo uliopita dhidi ya Mwadui FC.

Kukosekana kwake kutampa nafasi Mganda Emmanuel Okwi kucheza sambamba na Meddie Kagere, kinara wa mabao kwenye ligi akiwa amefunga mabao manne.

Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems anatarajiwa kuendeleza utamaduni wake wa kutumia washambuliaji wawili huku viungo Cleotus Chama na Shiza Kichuya wakitarajiwa kushirikiana na washambuliaji hao.

Licha ya kutoanza vyema msimu, Kichuya amekuwa na bahati ya kipekee kila Simba inapocheza na Yanga. Kichuya ameifunga Yanga mabao matatu katika michezo minne iliyopita baina ya timu hizo.

Viungo wakabaji James Kotei na Jonas Mkude watakuwa na kazi ya kuwadhibiti viungo wa Yanga Papi Tshishimbi, Feisal Salum na Ibrahim Ajib.

Kotei huenda akapewa kazi maalum ya kumuweka chini ya ulinzi Ajib anayeonekana kuwa katika kiwango bora msimu huu.

Safu ya ulinzi ya Simba haitarajiwi kuwa na mabadiliko. Erasto Nyoni na Paschal Wawa wamekuwa na maelewano mazuri sana tangu waanze kucheza pamoja.

Huku upande wa kulia Shomari Kapombe akitarajiwa kuongoza mashambulizi wakati kushoto Mohammed Hussein akitarajiwa kuanza mbele ya Asante Kwasi ambaye majeruhi yamemfanya akose michezo ya mwanzo wa msimu.

Misimu ya hivi karibuni Simba imekuwa ikitawala mchezo wa watani wa jadi kutokana na ubora wa kikosi chake.

Simba ina matumaini makubwa ya kuibuka na ushindi kwenye mchezo wa leo unaotarajiwa kuanza saa 11 jioni.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
10h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
16h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
18h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
22h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
22h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
22h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’