Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera ameifanyia 'ushushushu' Rayon Sports na amebaini klabu hiyo inafungika kama vijana wake watazingatia maelekezo yake.
Zahera alibaki na nusu ya kikosi cha Yanga jijini Dar es salaam huku nusu nyingine ikisafiri Mbeya, Morogoro kukamilisha ratiba ya michezo ya ligi kuu ya Vodacom.
Zahera amesema amekuwa akiwafuatilia Rayon Sports, amekiri wana kikosi kizuri kisichopaswa kubezwa lakini anaamini Yanga iko kwenye nafasi nzuri ya kupata ushindi keshokutwa.
Yanga iliyobaki jijini Dar es salaam imekuwa ikijifua kwenye uwanja wa Polisi.
Hata hivyo mazoezi yaliingia dosari jana baada ya uwanja huo kujaa maji kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar es salaam.
Wachezaji waliokuwa na kikosi cha Yanga ambacho kilichapwa bao 1-0 na Mtibwa Sugar mkoani Morogoro jana watajumuika na wenzao kuendelea na maandalizi ya mchezo huo.
Wachezaji wengine Ibrahim Ajib, Haji Mwinyi na Kelvin Yondani ambao walikuwa na udhuru nao wanatarajia kujiunga wenzao leo kulingana na Meneja wa Yanga Hafidh Saleh.

ADVERTISE HERE