Katibu Mkuu Yanga amjulia hali Manara

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
25 Sep 2018
Katibu Mkuu Yanga amjulia hali Manara
Jana Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga Omari Kaya alifika nyumbani kwa Mkuu wa Habari wa Simba Haji Manara kumjulia hali kutokana na kuugua maradhi ya tumbo.

Manara aliugua ghafla mkoani Shinyanga juzi alikokuwa na klabu ya Simba ambapo alilazimika kukimbizwa Hospitalini ambapo jana alirejea jijini Dar es salaam kwa matibabu zaidi Hospitali ya Muhimbili.

Baada ya kutibiwa jana hiyo hiyo aliruhusiwa kurudi nyumbani.

Manara amesema ujio wa kiongozi huyo wa Yanga nyumbani kwake unadhihirisha uhusiano mwema uliopo baina ya Simba na Yanga.

Amesema vilabu hivyo havina uaduia kama inavyochukuliwa na baadhi ya mashabiki.

"Sijui lini ntaeleweka ninaposema Simba na Yanga si maadui wala mahasimu, fikiria miongoni mwa watu wa mwanzo kuja kwangu kuniona baada ya kutoka hospitali ni swahiba wangu ambaye ndiyo Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga Omar Kaya.

"Tumeongea na kutaniana lakini pia kushauriana yenye faida kwa mpira wa Tanzania.

"Mashabiki maandazi jifunzeni kwetu na kwa wachezaji, sisi hatuna uadui, msitukanane wala kukunjana, charurareni bila kugombana" amesema
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
3h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
5h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
6h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
8h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
12h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’