FT : Prisons 2-0 Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
11 May 2018
FT : Prisons 2-0 Yanga
Yanga imevuliwa rasmi ubingwa wa ligi kuu ya Vodacom na wapinzani wake Simba baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa Prisons kwenye mchezo wa ligi hiyo uliopigwa katika dimba la Sokoine mkoani Mbeya.

Mabao ya Prisons yalipatikana kwenye kipindi cha pili yakifungwa na Eliuta Mpepo kwa njia ya mkwaju wa penati kwenye dakika ya 58 na Salum Bosco aliyefunha bao la pili kwenye dakika ya 85.

Yanga ilikwenda Mbeya ikiwa na kikosi cha wachezaji 13 pekee ambapo ilikuwa na wachezaji wawili wa akiba.

Uamuzi wa kupeleka idadi hiyo ulipendekezwa na Kocha Mpya wa timu hiyo Mwinyi Zahera aliyetaka wachezaji wa kikosi cha kwanza wabaki jijini Dar es salaam kuundelea na maandalizi ya mchezo wa kombe la shirikisho dhidi ya Rayon Sport, May 16 2018.

Matokeo hayo yameipa rasmi Simba ubingwa wake wa kwanza baada ya kusubiri kwa misimu mitano.

Yanga imebakisha michezo mitano ambayo ikishinda yote itafikisha alama 63 wakati Simba tayari ina alama 65.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
4h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
8h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
13h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
13h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
16h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’