Licha ya Shirikisho la soka nchini (TFF) kutangaza kumfungia Meneja wa Simba Robert Richard kwa mwaka mmoja, bado klabu ya Simba haijapokea barua rasmi kutoka TFF.
Juzi Kaimu Rais wa Simba Salim Abdallah 'Try Again' alisema klabu hiyo itakata rufaa kupinga kifungo hicho cha mfanyakazi wake ambacho kinaambatana na faini ya Shilingi Milioni nne.
Uongozi wa Simba umeeleza kuisubiri barua hiyo kwa ajili ya kuanza mchakato wa rufaa.
Kikosi cha Simba kimesafiri mkoani Mtwara bila Meneja wake huyo ambaye ameanza kutumikia adhabu.

ADVERTISE HERE