Mshambuliaji wa Yanga, Emmanuel Martin amesema anaamini furaha ya mashabiki wao kwa msimu huu ni wao kufanya vizuri katika Kombe la Shirikisho Afrika ambapo May 06 itaanzia ugenini dhidi ya USM Alger.
Martin amekiri anatambua mashabiki wa Yanga, wana maumivu ya kufungwa na watani wao wa jadi Simba, hivyo ili kuwapunguzia adhabu hiyo ni kutumia fursa ya mashindano ya kimataifa.
"Mechi ya watani inaumiza kutokana na utani unakuwepo baada ya mechi kumalizika, hatukupenda matokeo yawe hivi ila hatuna budi kupambana na kuangalia ya mbele.
"Naamini tukifanya vizuri kimataifa, itafuta kila kitu kwani tutakuwa tumeweka historia ya aina yake ambayo haitafutika vizazi na vizazi vitakavyokuja nyuma yetu," alisema Martin.
Mwanaspoti

ADVERTISE HERE