Baada ya mchezo dhidi ya Namungo Fc ambao Simba iliibuka na ushindi wa mabao 3-2, uongozi wa klabu hiyo uitoa mapumziko ya wiki moja kwa wachezaji ambao hawakuitwa kwenye majukumu ya timu za Taifa.
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba Ahmed Ali amesema wachezaji wanatarajiwa kurejea kambini Novemba 09 kuanza maandalizi ya mechi za ligi zinazofuata pamoja na ligi ya mabingwa.
Ahmed amesema uongozi unafanya mchakato wa kambi maalum kama walivyofanya awamu iliyopita ili kujiandaa vyema kwa mechi zinazofuata ambapo mchezo dhidi ya Orlando Pirates ndio utakaofungua hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa.
Baada ya mapumziko, klabu ya Simba huenda ikaelekea nchini Kenya kuweka kambi ya muda mfupi ambapo wamealikwa kushiriki kumbukumbu ya mwaka mmoja wa kifo cha Raila Odinga Novemba 15 kwa mchezo wa kirafiki dhidi ya Gor Mahia.