Yanga ya Ramovic lazima uzuie na kushambulia

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
2 Dec 2024
Yanga ya Ramovic lazima uzuie na kushambulia

Kocha Mkuu wa Yanga Sead Ramovic juzi alimfanyia mabadiliko Stephane Aziz Ki dakika 5 tu baada ya kuanza kipindi cha pili cha mchezo wa ligi kuu dhidi ya Namungo Fc uliopigwa uwanja wa Majaliwa, Ruangwa na Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 2-0

Clatous Chama ndiye aliyeingia kuchukua nafasi ya Aziz Ki na kwa kiasi kikubwa Chama aliongeza kasi ya mashambulizi akitoa pasi ya bao la pili lililofungwa na Pacome Zouzoua

Kilichowafurahisha wengi ni jinsi Chama alivyokuwa akiongoza kufanya 'pressing' dhidi ya walinzi wa Namungo Fc, yakiwa ni mabadiliko makubwa ya aina ya uchezaji wake

Akizungumzia sababu ya mabadiliko aliyofanya mapema kwa kumtoa Aziz Ki, Ramovic alisema kila mchezaji anahitaji kufanya kazi timu inapokuwa na mpira na hata bila ya mpira

Ramovic alisisitiza falsafa yake ni kushambulia na kuzuia kwa pamoja kuwanyima wapinzani nafasi ya kumiliki mpira kwa muda mrefu

"Aziz Ki alifanya kazi nzuri katika kipindi cha kwanza hasa timu inapokuwa haina mpira, tunataka kuona kila mchezaji anashiriki kikamilifu pale tunapotafuta mpira"

"Chama alipoingia nae amefanya kazi nzuri, ametengeneza bao la pili, hawa ni wachezaji wa daraja la juu ambao najivunia kuwa nao katika kikosi," alisema

Juzi Yanga ilionyesha mabadiliko ya kiuchezaji hasa ilipokuwa haina mpira. Mawinga na viungo wote walirudi chini kuzuia na kushambulia kwa haraka walipopata mpira

Mabao yote mawili yalikuwa ni matokeo ya 'transition' baada ya Yanga kupora mpira na kushambulia kwa haraka

Kennedy Musonda alifunga bao la kwanza baada ya pasi ya Maxi Nzengeli, mashambulizi yakianzia kwa Pacome Zouzoua aliyepora mpira upande wa kulia

Bao la pili alilofunga Pacome lilianzia nyuma ambapo Pacome alishiriki tena katika ulinzi kabla ya kutoa pasi kwa Duke Abuya ambaye alimpasia Chama aliyemtengea Pacome aliyekimbia kutoka nyuma na kufunga bao bora la mchezo huo

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Aziz Ki ameanza kwa kusuasua lakini namba zinaongea
Aziz Ki ameanza kwa kusuasua lakini namba zinaongea
6m ago
READ MORE β†’
Nini matarajio Fadlu kutua Yanga?
Nini matarajio Fadlu kutua Yanga?
2h ago
READ MORE β†’
Maxi na msimu wa maajabu Yanga
Maxi na msimu wa maajabu Yanga
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Ijumaa, Novemba 06 2026
Magazeti ya leo Ijumaa, Novemba 06 2026
6h ago
READ MORE β†’
Abuya, Yao warejea mazoezini baada ya kupona majeraha
Abuya, Yao warejea mazoezini baada ya kupona majeraha
16h ago
READ MORE β†’
Mpango wa kumshusha Ramovic umekwama, Yanga yarudi kwa Fadlu
Mpango wa kumshusha Ramovic umekwama, Yanga yarudi kwa Fadlu
21h ago
READ MORE β†’
Dladla amejihakikishia nafasi yake Yanga
Dladla amejihakikishia nafasi yake Yanga
1d ago
READ MORE β†’
Happy Birthday Mwamnyeto
Happy Birthday Mwamnyeto
1d ago
READ MORE β†’
Novemba 5 itaendelea kukumbukwa na Wananchi
Novemba 5 itaendelea kukumbukwa na Wananchi
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi Novemba 05 2026
Magazeti ya leo Alhamisi Novemba 05 2026
1d ago
READ MORE β†’