Washambuliaji hatari wa Simba Meddie Kagere na Emanuel Okwi wamerejea nchini na kuungana na wenzao wanaoendelea na mazoezi kwenye uwanja wa Boko Veterans jijini Dar es salaam.
Okwi alikuwa Uganda kwa majukumu ya timu ya taifa ya nchini hiyo iliyolazimishwa suluhu ya bila kufungana na Tanzania wakati Kagere alikuwa Rwanda akifunga bao la kufutia machozi wakati Rwanda ilipochapwa mabao 2-1 na Ivory Coast.
Cletus Chama aliyekuwa Zambia alitarajiwa kuwasili leo huku Juuko Murshidi na Haruna Niyonzima wakiendelea kukosekana.
Simba inatarajiwa kwenda mkoani Mtwara kucheza na Ndanda FC katika mchezo utakaopigwa Jumamosi ijayo, Septemba 15 kwenye uwanja wa Nagwanda Sijaona.

ADVERTISE HERE