Tutapambana tuvuke mtoano - Barker

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
1h ago
Tutapambana tuvuke mtoano - Barker

Kocha Mkuu wa Simba Steve Barker amesema licha ya ugumu wa kundi ambalo timu hiyo imepangwa katika ligi ya mabingwa, dhamira kuu ni kuvuka hatua hiyo kwenda kwenye mtoano.

Droo ya hatua ya makundi ya CAFCL msimu huu ilifanyika jana nchini Misri Simba ikipangwa kundi C pamoja na timu za RS Berkane, Orlando Pirates na Colombe.

Akizungumzia kundi hilo na matarajio yake, Barker alisema watakwenda kukutana na wapinzani ambao baadhi yao tayari wanawafahamu vyema.

Amesema ni kundi litakalokuwa na upinzani mkali lakini ili kuweza kusonga mbele katika michuano hii lazima kuvuka hatua ya makundi bila ya kujali upinzani ambao watakabiliana nao.

"Ni kundi gumu, timu zote ziko imara. Nawafahamu vyema RS Berkane nilikutana nao wakati niko Stellenbosch ni timu nzuri."

"Pia tunakwenda kukutana na Orlando Pirates, nimekutana nao mara nyingi Afrika Kusini, ni timu nzuri, kila mmoja anafahamu kile wanachoweza kufanya katika mashindano kama haya"

"Pia kuna timu mpya kwenye kundi letu Colombe kutoka Cameroon nafikiri nao watatoa ushindani."

"Lakini jambo muhimu ni kuwa ili uweze kusonga mbele lazima uvuke hatua ya makundi bila ya kujali upinzani utakaokutana nao."

"Lengo letu kuu ni kuvuka hatua hii, tuna dhamira kubwa kufika hatua ya mtoano. Tunaamini katika uwezo wetu kama timu na malengo makubwa tuliyojiwekea msimu huu, tunataka kufika mbali," alisema Barker

Simba imewahi kukutana na Orlando Pirates kwenye robo fainali ya kombe la Shirikisho mchezo ukimalizika kwa sare ya bao 1-1 baada ya dakika 180 za mechi mbili Pirates wakifuzu nusu kwa ushindi wa mikwaju ya penati.

Ni msimu mmoja tu umepita tangu Simba wakutane na RS Berkane kwenye fainali ya michuano hiyo hiyo na Berkane kuibuka na ushindi wa jumla wa mabao 3-1 na kutwaa taji hilo visiwani Zanzibar.

Wakati ni nafasi kwa Wekundu wa Msimbazi kulipa kisasi dhidi ya wapinzani wake hao.

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mangungu aibuka, apinga mchakato wa uchaguzi Simba
Mangungu aibuka, apinga mchakato wa uchaguzi Simba
17m ago
READ MORE β†’
Matchday; Fountain Gate vs Simba, NBC PL
Matchday; Fountain Gate vs Simba, NBC PL
3h ago
READ MORE β†’
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
4h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
6h ago
READ MORE β†’
Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
20h ago
READ MORE β†’
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
21h ago
READ MORE β†’
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
1d ago
READ MORE β†’
Makundi CAFCL kujulikana leo
Makundi CAFCL kujulikana leo
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
1d ago
READ MORE β†’
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
1d ago
READ MORE β†’