Matchday : Yanga vs Al Hilal, CAF CL - R1

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
26 Nov 2024
Matchday : Yanga vs Al Hilal, CAF CL - R1

Hatimaye burudani ya ligi ya mabingwa barani Afrika imerejea! leo mechi za hatua ya makundi zinaanza kupigwa katika nchi mbalimbali

Miamba 16 bora zaidi barani Afrika inaanza kampeni ya kulisaka taji la CAF CL na kubeba kitita cha takribani Tsh Bilioni 10

Mabingwa wa Tanzania Bara Yanga ambao wanaiwakilisha nchi katika michuano hiyo, wanaanzia nyumbani kwa mchezo dhidi ya Al Hilal utakaopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa, saa 10 jioni

Mechi ngumu inayotarajiwa kuwa na upinzani mkali lakini matokeo pekee ambayo Yanga inahitaji katika uwanja wa nyumbani ni ushindi

Silaha kuu ya kufanikiwa katika michuano hii ni kuhakikisha unatumia vyema uwanja wa nyumbani na hivyo ushindi kwa Yanga leo ni kipaumbele

Utakuwa mchezo wa kwanza kwa kocha Sead Ramovic ambaye ana takribani siku 9 tangu achukue majukumu ya kukinoa kikosi cha Yanga baada ya Miguel Gamondi kusitishiwa mkataba

Akizungumza katika Mkutano na Wanahabari jana, Ramovic aliwataka mashabiki wa Yanga kujitokea kwa wingi katika mchezo huo huku akiahidi timu yake kucheza kwa ari kusaka ushindi

Ramovic alisema anajivunia kuifundisha Yanga yenye wachezaji wenye vipaji na matarajio yake ni kuona leo wanaanza vyema kampeni ya kusaka ubingwa wa Afrika

Kila la kheri Wananchi...!

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
1h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
6h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
6h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
10h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’