Baada ya kufuzu hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa barani Afrika (CAFCL) hapo jana, kikosi cha Simba hakina muda wa kupotez kwani leo wameondoka jijini Dar es salaam kuelekea Manyara tayari kwa mchezo wa ligi kuu dhidi ya Fountain Gate.
Mchezo huo unatarajiwa kupigwa keshokutwa Jumatano, Oktoba 28, 2026 katika uwanja wa Tanzanite Kwaraa
Simba inayoongoza msimamo wa Ligi Kuu kwa kuwa na pointi 24 inaelekea kwenye mchezo huo ikiwa na lengo la kuendelea kujiimarisha kwenye nafasi hiyo.

ADVERTISE HERE