Kikosi cha Yanga chini ya kocha Sead Ramovic kinaendelea na maandalizi ya mchezo wa kwanza hatua ya makundi ligi ya mabingwa barani Afrika dhidi ya Al Hilal
Yanga itakuwa mwenyeji wa Al Hilal siku ya Jumanne, Novemba 26 katika mchezo utakaopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa
Yanga inakwenda katika mchezo huo ikiwa na ari na morali kubwa, tangu Yanga iliporejea katika michuano ya CAF msimu wa 2022-23, takwimu zinawapa Wananchi jeuri ya kwenda kuwakabali Al Hilal wakiwa kifua mbeleΒ
Katika mechi ambazo Yanga imecheza nyumbani katika mashindano ya CAF tangu 2022-23,Β imepoteza mchezo mmoja tu ambao ulikuwa wa fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya USM Alger ya Algeria.
Katika msimu wa 2022-2023 ambao Yanga ilicheza kombe la Shirikisho, ilishinda mechi zote tatu katika hatua ya makundi na ikatoka sare mechi moja raundi ya pili robo fainali dhidi ya Rivers United
Msimu uliopita Yanga ilitoka sare mechi moja nyumbani katika hatua ya makundi dhidi ya Al Ahly na kushinda mechi zilizofuata dhidi ya Medeama na CR Belouizdad
Ikatoka suluhu ya bila kufungana dhidi ya Mamelodi Sundowns na kuondoshwa kwa mikwaju ya penati katika hatua ya robo fainali
Mchezo dhidi ya Al Hilal una umuhimu wa kipekee kwa Yanga kushinda ili kumaliza jinamizi la kupoteza mechi ya kwanza katika hatua ya makundi
Pia hii inaweza kuwa mechi ya kisasi kwa Yanga kwani 2022-23 Yanga ilicheza kombe la Shirikisho baada ya kuondoshwa na Al Hilal katika ligi ya mabingwa kwa kufungwa mabao 2-1 matokeo ya aggregate baada ya mechi zote mbili
Sare ya bao 1-1 katika mchezo uliopigwa Dar na kupoteza kwa bao 1-0 katika mchezo wa pili uliopigwa Sudan kabla ya vita ya wenyewe kwa wenyewe iliyopelekea Al Hilal kuhamia Mauritania
Yanga SC Stories