Zikiwa zimebaki siku mbili kabla ya kufungwa uchukuaji fomu za kuwania nafasi mbalimbali za uongozi Simba hadi jana hakukuwa na mwanachama yeyote aliyejitokeza kuchukua fomu za kuwania Urais.
Mwenyekiti wa Uchaguzi, Boniface Lyamwike alisema hadi jana mchana ni mjumbe mmoja tu aliongezeka baada ya juzi kuwa na idadi ya wajumbe sita.
Alisema pia katika akidi ya kugombea nafasi ya ujumbe katika klabu hiyo ambao inataka wajumbe watano wanne wanaume na mmoja mwanamke hadi sasa hakuna mwanamke hata mmoja aliyejitokeza kuchukua fomu.
"Nafikiri siku ya leo (jana) bado haijaisha hadi jioni huenda akajitokeza mwanachama ambaye anatamani kuwania nafasi ya Urais, siku mbili zilizobaki mbona ni nyingi sana wito wangu kwa wanachama ni kuwaomba kujitokeza kwa wingi kwa lengo la kuhakikisha klabu yetu inafika mbali zaidi kimaendeleo," alisema.
Utoaji fomu za kuwania nafasi za ujumbe na urais katika uchaguzi wa klabu ya Simba unaotarajiwa kufanyika Novemba 3 mwaka huu linatarajiwa kufungwa Jumatatu.
Mwanaspoti

ADVERTISE HERE