April 29 ni siku ya kumshikisha adabu mtani

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
26 Apr 2018
April 29 ni siku ya kumshikisha adabu mtani
Hiyo ndio kauli mbiu ya kila Mwana Jangwani kuelekea mchezo dhidi ya Simba utakaopigwa April 29 kwenye uwanja wa Taifa.

Ili ushindi upatikane mapema ni muhimu tuhamasishane kuhakikisha tunafurika kwa wingi uwanja wa Taifa huku tukiwa tumevaa jezi za Yanga.

Yanga ndio klabu yenye mashabiki wengi Tanzania hilo halina ubishi, tulidhihirishe Jumapili pale uwanja wa Taifa.

Yanga haijawahi kuihofia Simba, kuongoza kwao ligi hakumaanishi kuwa wao ni timu bora.

Hebu mjiulize, pamoja na mbwembwe zote wamepata nini kwenye michuano ya Kimataifa?

Michuano ya CAF CC ambayo walikuwa wamewekeza sana wameondolewa kwenye raundi ya kwanza lakini michuano hiyo hiyo Yanga imetinga hatua ya makundi licha ya changamoto kibao ilizopitia.

Kama Simba haikushinda kwenye mchezo wa raundi ya kwanza wakati huo Yanga ikiwa haiko sawa, watashindaje sasa?

Jumapili ndio siku ya kuwaziba midomo, muhimu twendeni uwanja wa Taifa tukawape sapoti vijana, hawatatuangusha

Ushindi kwenye mchezo wa Jumapili utairejesha rasmi Yanga kwenye mbio za ubingwa.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
4h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
7h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
12h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
12h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
16h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’